Samuel Eto'o anaweza kuondoka katika klabu ya Sampdoria wiki tu baada ya kujiunga nayo kutoka klabu ya Everton, na
hiyo yaarifa ni kulingana na ripoti kutoka nchini Italia.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alicheza mechi yake ya kwanza na Sampdoria katika Serie A akiingia kama mbadala dakika ya 71 wakati timu hiyo ilipopokea kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya Torino siku ya Jumapili.
Meneja wa Sampdoria Sinisa Mihajlovic hatimaye aliamuru kikosi kuhudhuria mazoezi ya ziada - na hivyo kuzua maswali kwa nyota huyo wa zamani wa Cameroon Eto'o, ambaye inadaiwa alikataa.
Mihajlovic alisema: "hakukuwa na majibizano na Eto'o, kwa sababu rahisi kwamba kulikuwa na watu wawili wanaongea, sikuweza kumwona tena baada ya mazoezi ya asubuhi wala.., mimi kuongea naye."
"Sijui kwa nini aliondoka, wala sijui mipango ipi klabu imepanga kufanya kwa sasa. Yote ni kwamba mchezaji hakunipa maelezo yoyote. Mimi nafikiria ni ukosefu mkubwa wa heshima kwangu na kikosi. "
klabu imekataa kuthibitisha tukio hilo, ambalo ripoti pia inadai tukio hilo linaweza kusababisha kusitisha mkataba wa Eto'o baada ya wiki moja tu.
Badala yake, rais wa Sampdoria Massimo Ferrero alisema: "kulikuwa na tofauti ya maoni tu, na kwa kweli ni jambo moja dogo mno,Sisi tuko shwari, Sampo iko imara sana..." alisema
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments