Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:MSIKILIZE MRISHO NGASSA AKIZUNGUMZIA JUU KUKATA FEDHA ZAKE

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Feb.10,2015 SAA 01:46 USIKU
Siku ya jumanne tarehe 10 Feb.2015 Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Mrisho Ngasa alizungumza na waandishi wa
habari na kuiomba klabu yake kuweza kumlipia deni analodaiwa benki ili aweze kucheza kwa bidii katika klabu hiyo.
Kama utakuwa unakumbuka Ngassa aliamriwa kulipa deni la Sh 45 milioni kwa kosa la kujiunga na Yanga bila kufuata utaratibu akitokea Simba, hivyo , kwa makubaliano, analilazimika kukatwa Sh500,000 (wastani wa dola 280) kila mwezi kutoka katika sehemu ya mshahara wake anaoupata kutoka Yanga ili kulipa deni.
Mrisho Ngassa akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
Ngassa pia aliripotiwa kusema kuwa hali yake ya kifedha “financial status” ni mbaya na kushindwa kucheza vizuri, na kuiomba Yanga kuangalia namna ya kumsaidia kulipa ili aweze kubakiwa na fedha za kutosha.
MSIKILIZE ZAIDI NGASSA AKIZUNGUMZA,AKIANZA NA SWALA LA KWENDA AFRIKA KUSINI
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, alisema benki , baada ya kukata 500,000, ililazimika kuchukua mshahara wote wa Ngassa katika miezi ya hivi karibuni ili kufidia deni analodaiwa baada ya uongozi uliopita wa klabu hiyo kushindwa kupitisha benki mshahara wake kwa muda unaokisiwa kuwa ni mwaka mmoja, hivyo kutolipa kwa mujibu wa makubaliano na benki kulazimika kumuacha mchezaji huyo bila senti.
Uongozi wa klabu ya Yanga umeahidi kumlipia Ngassa deni hilo
MSIKILIZE ZAIDI JERRY MURO AKIZUNGUMZA
 KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments