Ticker

6/recent/ticker-posts

LIGI KUU TZ BARA:MATOKEO AZAM FC,YANGA,MTIBWA SUGAR,MBEYA CITY NA TANZANIA PRISONS YAKO HAPA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.NOV.08,2014 SAA 03:30 USIKU

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara imeendelea Leo hii  (Novemba 8, 2014) kwa kupingwa
michezo mitano katika viwanja tofauti,huku hali ikiwa si hali kwa timu nyingine.


Katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kulikuwa na mechi kati ya Yanga na Mgambo Shooting na matokeo ya mchezo huo ni kwamba timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 0.



Hadi mapumziko ya mchezo huo timu hizo mbili zilikuwa hazijafungana.

kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kushambuliana lakini,mgambo Jkt walipata pigo kwa beki wao Salim Kipaga kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kuzozana na Mrisho ngassa





 Yanga walipata mabao mawili kupitia kwa Saimon Msuva dakika ya 74 na katika dakika ya mwishoni ya mchezo huo.

Uwanja wa Chamazi ulikuwa na mechi kati ya Azam na Coastal Union, na matokeo ya mchezo huo, Azam wakachomoza na ushindi wa mabao 2-0, na mabao yao yamefungwa na Kipre Herman TChetche pamoja na Shomary Kapombe.

Mechi ya Mtibwa Sugar na Kagera Sugar imelazimika kuahilishwa hadi siku ya kesho hasubui baada ya mvua kunyesha katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro,lakini mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu ya Mtibwa Sugar ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0,siku ya kesho mchezo huo utaendelea kwa dakika 45 zilizosalia.

Mbeya City imeendeleza Rekodi ya kufanya vibaya katika msimu huu,kwa kukubali kufungwa 1-0 na timu ya Stand United katika mchezo uliopigwa katika dimba la Kambarage mkoani Shinyanga.

Mechi nyingine imepigwa katika dimba la Jamuhuri mkoani Morogoro kati ya timu ya Polisi Morogoro na timu ya Tanzania Prisons,huku timu ya Polisi Morogoro ikiibuka na Ushindi wa 1 -0.

KESHO JUMAPILI

Simba - Ruvu Shooting = TAIFA,JIJI DAR ES SALAAM

JKT RUVU - NDANDA FC = AZAM COMPLEX, JIJI DAR ES SALAAM

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo ) 

Post a Comment

0 Comments