Kundi lililojipatia umaarafu kwa ushangiliaji kwa timu ya Simba la mpira na maendeleo lililopewa jina la UKAWA,limejikuta katika
wakati mgumu mara baada ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya timu ya Simba na Ruvu Shooting kumalizika kwa timu ya Simba kuibuka na ushindi wa 1-0.
wakati mgumu mara baada ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya timu ya Simba na Ruvu Shooting kumalizika kwa timu ya Simba kuibuka na ushindi wa 1-0.
Mashabiki hao wa Simba ambao wamefutiwa uanachama kwa kwenda mahakamani,mara nyingi huwa wanahusishwa na matokeo ya sare yaliyokuwa yakiiandama klabu hiyo, yenye makao yake makuu katika mtaa wa Msimbazi jijini Dar es salaam.
UKAWA walilazimika kuchukuliwa na polisi pamoja na wanausalama walioko katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam,mara baada ya taarifa kuwepo kuwa huenda wakavamiwa kisha kupigwa na mashabiki waliokuwa na uanachama wa klabu ya Simba,kwa kuwa kundi hilo la UKAWA huwa linahusishwa kwa kutabili matokeo ya Sare ya Klabu hiyo.
Polisi wakiwaambia UKAWA waingie ndani ya uwanja |
Jeshi la polisi lililazimika kuwalinda UKAWA mpaka nje |
Jeshi la Polisi lililazimika kuwalinda UKAWA,na kuwaambia waingie ndani ya uwanja,kisha kuwasindikiza mpaka nje ya uwanja na kuwapatia usafiri na kuwasindikiza mpaka katika makao yao makuu.
Wanausalama wakiwapatia usafiri UKAWA |
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo )
0 Comments