Ticker

6/recent/ticker-posts

STEPHEN KESHI AFUTWA KAZI NIGERIA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.OCT.16,2014 SAA 01:47  USIKU

Mabingwa wa Afrika Nigeria wamemuachisha kazi kocha wa kikosi chao cha kandanda, Stephen Keshi licha ya
kuwaongoza kukomoa Sudan 3-1 kwenye mechi ya kufuzu fainali za mwaka ujao Jumatano jijini Abuja.
Shirikisho la mpira wa miguu la taifa hilo, NFF lilitangaza baada ya mkutano wa dharura kuwa mwalimu wa zamani Shuaibu Amodu atachukua hatamu za muda huku wakitafuta kocha wa kigeni kuchukua uongozi wa kudumu.
Stephen Keshi
Super Eagles walipanda hadi nafasi ya tatu na alama nne na kufufua matumaini yao kufuzu kutetea taji la Kombe la Mataifa ya Afrika waliloshinda mwaka jana chini ya Keshi kufuatia ufanisi wao dhidi ya Sudan baada ya kuanza mechi wakivuta mkia Kundi D baada ya kushindwa mara mbili na kutoka sare moja.
Hatima ya Keshi ilianza kujadiliwa tangu mwisho wa Kombe la Dunia nchini Brazil mwezi Julai baada ya kuongoza timu hiyo kufuzu awamu ya miondoano ya shindano hilo.
Uhasama kati yake na nyota wakuu wa timu hiyo, Emmanuel Emenike, Peter Odemwingie na Ikechukwu Uche ulipunguza umaarufu wake miongoni mwa wachezaji baada ya kuendelea kuhudumu licha ya kandarasi yake kuisha kufuatia Kombe la Dunia.
“Keshi na kitengo chake cha ufundi wameongoza Nigeria kufika ngazi za utukufu lakini kwa maslahi ya kandanda ya Nigeria na hamu ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2015, kamati (tawala) imeamua kuwaachisha kazi mara moja,” taarifa ya NFF ilisema.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
Chanzo:super sport

Post a Comment

0 Comments