Ticker

6/recent/ticker-posts

EXCLUSIVE:MCHEZAJI WA WEST BROMWICH STEPHANE SESSEGNON AZUNGUMZIA SWALA KUBANIWA WACHEZAJI WA AFRIKA,PAMOJA NA MECHI YA KESHO DHIDI YA STARS

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.OCT.11,2014 SAA 09:31 MCHANA 

Stephane Sessegnon akizungumza hii leo

Naodha wa kikosi cha timu ya Benini Stephane Sessegnon amesema anaamini mchezo wa kesho wa kirafiki na timu ya
taifa ya Tanzania utakuwa mgumu,lakini amesisitiza kuwa lengo lake ni kushinda katika mchezo huo utakaopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Stephane Sessegnon akiwa katika klabu yake ya sasa West Bromwich Albion
Stephane Sessegnon akiwa  Paris Saint-Germain ya Ufaransa
Stephane Sessegnon akiwa Sunderland ya England 
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Stephane Sessegnon ambaye ni mchezaji wa West Bromwich Albion ambaye pia amechezea vilabu kadhaa vya ulaya kama Paris Saint-Germain ya Ufaransa na Sunderland ya England amesema haifahamu vizuri Timu ya Tanzania lakini lengo lao ni kushinda.

Akizungumzia swala linalosemekana kuwa wachezaji wa Afrika wanaocheza ulaya huwa hawajitumi katika timu zao za Taifa,Sessegnon amekiri kuwa tatizo hilo lipo kwa wachezaji wengi wanapokuja Afrika kwa sababu klabu wanazochezea huwa wanawapa masharti kwa kuhofia kuumia,lakini Sessegnon amesema yeye ni mpiganaji na kuahidi kesho atafanya vizuri katika timu yake ya Benini.

Akijibu swali la mwandishi wa habari za michezo,Mchezaji huyo wa West Bromwich Albion pia amezungumzia swala la wachezaji wengi wa Afrika kutopewa nafasi kama kutambuliwa na kupewa tuzo wanapofanya vizuri katika timu za ulaya,akisema hiyo ni hali ya kawaida hata yeye imemtokea akiwa Ufaransa na kusisitiza yeye hajali hilo kwani anachoangalia ni kufanya kazi.

Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Wachezaji wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli ya JB Belmont waliwasili Juzi (Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa nyakati tofauti.


Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake ya kwanza jana (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya mwisho leo (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.


Wachezaji walioko kwenye kikosi cha Benin ni Stephane Sessegnon (West Bromwich Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg, Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudou (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa).


Steve Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).


Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (USS Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments