Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Sept.22,2014 SAA 02:15 USIKU
Beki wa Arsenal Mathieu Debuchy atakuwa nje kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji juu ya kifundo cha mguu
ambapo alijeruhiwa katika mechi dhidi ya Manchester City.
Mfaransa huyo alitolewa nje dakika ya tisa kabla ya mchezo kumalizika katika uwanja wa Emirates baada ya kupata hitilafu katika mishipa ya kifundo cha mguu wake wa kushoto.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye alikuwa akiiwakilisha nchi yake katika fainali za Kombe la Dunia huko nchini Brazil, alikuwa akicheza mechi yake ya nne ya Ligi Kuu na Arsenal tangu ahamie kutoka katika klabu ya Newcastle mwezi Julai kwa ada ya £ 12million.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alikiri kuwa " Mathieu Debuchy amefanyiwa upasuaji na atakuwa nje kwa muda wa miezi mitatu".
Wenger pia amekiri kwamba, kuwa nje kwa mchezaji huyo ni pigo kwa Arsenal,lakini akasisitiza kuwa nafasi ya mchezaji huyo itazibwa na wachezaji wengine.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments