Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Sept.14,2014 SAA 03:11 USIKU
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Brazil Geilson Santos "Jaja" leo amewaonyesha wapenzi wa soka nchini nini kazi yake
uwanjani baada ya kuisadia Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku yeye akikwamisha mabao mawili safi mchezo uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijni Dar es salaam.
Young Africans ambayo ilikua ikicheza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya mashabiki wake zaidi ya elfu thelathini waliofurika kuwapa morali wachezaji, walitulia na kucheza soka tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho.
Kocha Mbrazil alianza na mfumo wa 4-5-1 walinzi Juma Abdul Oscar Joshua, Kelvin Yondani na Nadri Haroub "Canavvaro", mbele yao wakicheza viungo wa Ulinzi Mbuyu Twite na Said Juma "Makapu" wakisaidiwa na Haruna Niyonzima, Mrisho Ngasa na mbrazil Jaja akianza mshambuliaji peke yake.
Saimon Msuva alimaliza ndoto za timu ya timu ya Azam kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuipatia timu yake bao la tatu na ushindi na kuifanya Young Africans kuchukua Ngao ya Jamii kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake huku Simba wakiwa wamechukua mara mbili na Mtibwa Sugar mara moja.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 - 0 Azam FC.
Mara baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Young Africans mbrazili Marcio Maximo amesema anawashukuru wachezaji wake kwa kucheza kwa kufuata maelekezo yake hali iliyoplekea kucheza soka safi la kuburudisha linaloambatana na ushindi.
Aidha Maximo amesema baada ya ushindi wa leo maandaliz ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar yataanza siku ya jumanne ambapo kwa kesho ametoa mapumziko kwa wachezaji wote pamoja na benchi la Ufundi.
Mwisho Maximo amewapongeza vingozi, waachezaji na washabik wa Young Africans kwa sapoti wanayoitoa kwa timu na kuomba wajitokeze kwa wingi pia mjin Morogoro mwishoni mwa wiki katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
Young Africans: 1. Deo Munish "Dida", 2. Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4. Nadir Haroub "Cananavao" (C), 5.Kelvin Yondani, 6.Mbuyu Twite, 7.Said Juma "Makapu"/Hassan Dilunga, 8.Haruna Niyonzima/Hamis Kizza, 9.Geilson Santos "Jaja"/Hussein Javu, 10.Mrisho Ngasa/Omega Seme, 11.Nizar Khalfani/Saimon Msuva/
Azam FC: 1.Mwadini Ali, 2.Shomari Kapombe, 3.Erasto Nyoni/Gadiel Michael, 4.David Mwantika, 5.Agrrey Morrsi, 6.Kipre Balou, 7.Himid Mao/Kelvin Friday, 8.Salum Abubakar, 9.Didier Kavumbag, 10.Kipre Tchetche/Ismail Diara, 11.Leonel st.Pres/Khamis Mcha
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments