Ticker

6/recent/ticker-posts

LIGI YA MABINGWA:JOSE MOURINHO AMETHIBITISHA HILI KUHUSU DIEGO COSTA NA DIDIER DROGBA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Sept.30,2014 SAA 10:45 ALFAJIRI

Jose Mourinho amethibitisha kuwa mshambuliaji Diego Costa ataanza katika kikosi cha Chelsea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Sporting Lisbon, lakini Didier
Drogba yeye atakuwa nje katika mchezo huo.

Bosi huyo wa The Blues Mourinho anatarajia Costa ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la misuli kuanza katika mchezo huo wa kundi G utakao pigwa katika dimba la Estadio Jose Alvalade leo usiku - pamoja na mchezo wa Ligi kuu na  Arsenal siku ya Jumapili.

Chelsea ilitoka sare ya kusikitisha (1-1) katika mechi ya kwanza Kundi G dhidi ya Schalke, na Costa ambaye amefunga mabao nane katika michezo sita ya Premier League, alicheza robo saa tu ya mwisho ya mechi hiyo ambayo ilishuhudia washambuliaji wa Chelsea kukosa makali. Drogba, ambaye bado ahajafunga bao tangu arudi Chelsea mara ya pili, ni mmoja wa waliopoteza nafasi nyingi. Loic Remy kufikia sasa yeye amefunga bao moja tangu ajiunge na Chelsea kutoka QPR.

"Diego ataanza," alisema Mourinho, ambaye alikuwa akizungumza usiku,siku moja kabla ya mchezo katika mji mkuu wa Ureno.
"Kuna hatari, ndiyo, lakini atacheza.tunadhani ni hatari na yeye atacheza.tunatumaini kila kitu kinaendelea vizuri na tunatumaini kutoka Jumanne hadi Jumapili atakuwa na kipindi cha kutosha kwa muda wa kurudi tena na kucheza dhidi ya Arsenal (katika Premier League)".
"Ni mchezo muhimu kwetu kesho, mchezo mgumu na naweza kuchezesha wachezaji wangu bora na timu nadhani ni timu bora tutajaribu kupata matokeo bora, si endi kufanya mabadiliko yoyote".
"si pumzishi watu,nafanya maamuzi, si fikirii kuhusu Arsenal - Nafikiria kuhusu Sporting na mimi nina kwenda kuanza na timu hiyo nadhani ni timu bora."
Loic Remy ni mtu pekee kama mbadala wa Costa katika kikosi cha Chelsea baada ya Drogba kukabiliwa na tatizo la ankle katika mazoezi.
"Drogba atakuwa nje kwa wiki kadhaa," Mourinho aliongeza.
"Alipatwa na tatizo katika mazoezi katika kifundo cha mguu.haikuwezekana kusafiri (kwanda Lisbon) na nafikiri haitawezekana kuwa vizuri siku ya Jumapili."

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments