Ticker

6/recent/ticker-posts

KUELEKEA LIGI KUU TZ:KOCHA MSAIDIZI WA YANGA SALVATORY EDWARD ATOA MTAZAMO WAKE

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Sept.19,2014 SAA 05:25  USIKU

Maandalizi ya ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Jumamosi hii septemba 20 yako katika hatua nzuri kwa

maana ya Viwanja,ambapo bodi ya Ligi Iko katika Ukaguzi wa mwishoni wa Viwanja.

Lakini kwa upande wa vilabu wanaitazamaje ligi hiyo?


Baada ya kuangalia klabu ya Azam fc na Coastal Union kutoka Tanga,leo tunaangalia klabu Yanga yenye makao yake makuu mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam,na Jamii na Michezo imezungumza na kocha msaidizi wa timu hiyo Salvatory Edward.
Kocha Marcio Maximo akumuelezea Jambo Mmoja wa wasaidizi wake Salvatory Edward (Picha na Othman Michuzi)
Kocha huyo ambaye anaamini michezo ni moja ya sehemu kubwa ya kukutanisha watu wa aina tofauti tofauti,amesema ligi ya mwaka huu itakuwa na ushindani mkubwa sana.

"Ligi ni ligi,haiangalii mtu aliyepanda daraja wala aliyekuwa katika mashindano,na huwezi kujua mpaka ligi itakapo anza kwa sababu kila mtu anapoingia katika Ligi dhumini lake ni kufanya vizuri na kupata ubingwa kwahiyo ushindani lazima utakuwepo" alisema Salvatory Edward.


Pia kocha huyo ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Timu hiyo amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa watafanya vizuri zaidi katika msimu huu.

"Malengo yetu ni kufanya Vizuri,ninaposema kuwa Ligi ni Ligi ninamaana kuwa kila timu ina nia ya kufanya vizuri,hakuna timu ambayo inashiriki Ligi na nia yao ni kufanya Vibaya,kila mtu ana nia ya kufanya vizuri kwaiyo ushindani utakuwepo" alifafanua Salvatory Edward

Salvatory Edward pia amewataka wanamichezo wote wazidishe umoja na ushirikiano kwani ndio kitu muhimu katika michezo.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments