NA MWANDISHI WETU, TANGA.IMEWEKWA.Sept.19,2014 SAA 06:46 USIKU
Maandalizi ya ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Jumamosi hii septemba 20 yako katika hatua nzuri kwa
maana ya Viwanja,ambapo bodi ya Ligi Iko katika Ukaguzi wa mwishoni wa Viwanja.
maana ya Viwanja,ambapo bodi ya Ligi Iko katika Ukaguzi wa mwishoni wa Viwanja.
Lakini kwa upande wa vilabu wanaitazamaje ligi hiyo?
Baada ya kuangalia klabu ya Azam fc,Leo tunaangalia klabu Coastal Union kutoka Tanga ambapo Kocha mkuu wa kikosi hiko Yusuph Chippo
amewapa mitihani mkubwa wachezaji wa kikosi hicho kuhakikisha wanapambana kufa
na kupona ili kuweza kuchukua pointi tatu dhidi ya Simba Jumapili wiki hii.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya pazia la michuano ya
Ligi kuu Tanzania bara kufunguliwa.
KOCHA CHIPO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI |
Chippo amesema maandalizi ya kuelekea mchezo huo kwa
wachezaji wake yanaendelea vizuri kwa wachezaji wote kuhudhuria kwenye mazoezi
ya timu hiyo ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya soka Disuza jijini Tanga na Popatlaly
Licha ya mazoezi hayo ya uwanjani wachezaji hao
wamekuwa wakiingia gym asubuhi kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort huku walinda
milango wa timu hiyo wakifanya mazoezi maalumu ya kuwawezesha kuwa imara zaidi.
Chippo amesema timu hiyo itaingia uwanjani hapo
wakiwa na matumaini ya kupata ushindi wa aina yoyote ile ili kuweza kuanza ligi
kuu vema lengo likiwa kuanza mikakati yao ya kuwania taji hilo ambalo
linawaniwa na timu kumi na nne.
Hata hivyo Kocha huyo aliendelea kusisitiza nidhamu
na kujituma kwa wachezaji hao ili waweze kupata mafanikio kwa sababu hiyo ndio
silaha tosha ya kupata matokeo mazuri kwenye mechi yoyote ile.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments