Mshambuliaji wa England Daniel Sturridge amepelekwa kufanyiwa uchunguzi baada ya mchezaji huyo kujeruhiwa
katika mazoezi siku ya leo Ijumaa.
Chama cha Soka bado hakijafafanua juu ya kuumia kwake ,lakini wanasema Sturridge itakuwa akifanyiwa tathmini na wafanyakazi wa afya kutoka England baada ya kufanyiwa uchunguzi.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool mwenye miaka 25 alicheza kwa dakika 89 katika mchezo wa kirafiki walioibuka na ushindi wa bao 1 - 0 dhidi ya Norway katika uwanja wa Wembley siku ya Jumatano.
Vijana hao wa Roy Hodgson watakutana na Uswisi katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya kufuzu ya kombe la Ulaya 2016 siku ya Jumatatu.
Na beki wa England Gary Cahill pia amekosa katika mazoezi kutokana na tatizo la ankle lakini anatarajiwa kuwa fit na atakua sehemu ya kikao katika mazoezi ya siku ya kesho Jumamosi.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments