NA MWANDISHI WETU,TANGA.IMEWEKWA.Sept.26,2014 SAA 10:28 MCHANA
KLABU ya Coastal Union imelishauri shirikisho la soka
nchini(TFF) kuhakikisha wanakuwa wakali kwenye kidhitibi
vitendo vya
kishirikina ambavyo vinajitokeza kabla ya kuanza michezo wa Ligi kuu soka
Tanzania bara kwani hali hiyo inadumaza maendeleo soka hapa nchini
Kwa sababu hali hiyo isipodhibitiwa upo uwezekano
mkubwa wa timu za Tanzania kushindwa kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa
wanayocheza nje za nchini
Kauli hiyo imetolewa leo na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji wa Coastal Union, Albert Peter mara baada ya usiku wa jana saa saba
usiku mashabiki ambao inasadikika ni wa timu ya Mbeya City kumwaga madawa
kwenye kambi ya Coastal Union jambo ambalo sio zuri.
Mjumbe huyo ambaye pia ni Mkuu wa Msafara wa Coastal Union amesema jambo
hilo linapaswa kukemewa ikiwemo kuchukua hatua kali timu ambazo zitabainika
zimefanya mambo ya kishirikina ili kuweza kupata matokeo mazuri kwenye mechi
zao.
Amesema kuwa
jambo hilo la mashabiki kufanya vitendo vya kishirikina kabla ya mechi hi suala
ambalo sio zuri kwa sababu linapelekea kushusha kiwango cha soka hapa nchini
hivyo iwekwe sheria kali kwa timu itakaobaini imefanya hivyo kuchukulia hatua
ili kukomeza vitendo hivyo.
Licha ya hayo amesema kikosi cha timu hiyo
kimejipanga vizuri ili kuweza kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo yao
ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ili kuweza kuchukua ubingwa wa Ligi hiyo.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments