WANACHAMA wa Klabu ya Coastal
Union bado wameonyesha nia ya kutokumkubali Makamu Mwenyekiti wa
klabu,Steven Mguto hiyo na
kuomba uitishwe mkutano mkuu wa uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi mitatu ili
kuweza kuzipa mapengo ya nafasi zilizopo wazi.
Nafasi hizo ni Mwenyekiti na
Wajumbe wawili ili kuweza kuongeza nguvu katika utendaji wa klabu hiyo lengo
likiwa kuharakisha kasi ya maendeleo na ufanisi hasa kwa viongozi wa ngazi za
juu.
Hayo yalielezwa jana na Wanachama
hao wakati wa kikao cha pamoja mbele ya Mwanasheria kutoka ndani ya shirikisho
la soka nchini (TFF) anayeshughulikia masuala ya Uanachama, Eliud Msovela
wakati alipokuwa akipokea maoni ya wanachama wa timu hiyo.
Mmoja kati ya wanachama hao
Salim Perembo amesema kimsingi baada ya kufanyika uchaguzi huo na kupatikana
Mwenyekiti wa wajumbe hao itamuongezea nguvu kwenye safu ya uongozi kufanya
kazi zake ipasavyo na kwa ufanisi mkubwa kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya
timu hiyo.
Perembo amesema uchaguzi huo
kufanyika utatoa mwelekeo mzuri wa kuendelea kupata viongozi ambao watakuwa na
madaraka kamili hali itakayoongeza umakini na uwajibikaji kwenye utendaji wa
shughuli za siku kwenye klabu hiyo.
Naye mwanachama mwengine
Yunusu Makata ambaye mwenye kadi nambari 245 alisema kujazwa kwa nafasi za
uongozi zilizowazi utaiwezesha klabu hiyo kuimarika hasa kwenye eneo hilo na
hatimaye kuiwezesha kupata maendeleo kwa kuweka mipango imara itakayoleta
mafanikio siku za usoni.
Kwa upande wake mwanachama Salimu
Mazrui mwenye kadi namba 0201, alisema suala la uchaguzi huo ni la muhimu sana
kwa ajili ya kuimarisha safu za juu za uongozi ngazi ya klabu hiyo baada ya
kuonekana kushindwa kusimamia ipasavyo majukumu yao .
Alisema wanachama hao ndio
waliamua kukubaliana na kauli moja ya kusema kuwa Makamu Mwenyekiti huyo hafai
kuongoza kwenye klabu hiyo kutokana na kuvunja katiba kitendo ambacho
kimepeleka wanachama kukosa imani naye.
Hata hiyo mwanachama
mwengine,Hemed Mbaraka ,Coastal Union inaendeshwa na katibu yake lakini Steven
Mguto hafuati katia ua Coastal Union na sio muadilifu kwenye uongozi wake hivyo
yeye binafsi hana imani naye na kutaka
endele kuwepo kwenye nafasi hiyo hiyo ya kudumazwa mpaka atakapojirekebisha.
Awali akizungumza katika
mkutano huo, Msovela alisema kuwa klabu hiyo inatakiwa kuhakikisha inafanya marekebisho
ya katiba kwa sababu hilo ndio jambo ambalo linaokena halijakaa sawa sawa .
Alisema kama katiba hiyo ingekuwa
imerekebishwa inawezekana kumuwajibisha kiongozi wa ngazi za juu kwenye kamati ya maadili
kipindi anapofanya mambo yasiyokuwa mazuri ndani ya klabu badala ya kutumia neno
la kumdumaza.
0 Comments