Baada ya Libya kujitoa kuwa mwenyeji wa Fainali za Afrika (AFCON) za 2017, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
limealika nchi wanachama kuomba uenyeji wa fainali hizo.
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Agosti 24 mwaka huu) imeamua Tanzania kuomba uenyeji wa fainali hizo.
Tunatambua kuwa moja ya masharti ya kuandaa fainali hizo ni pamoja na nchi kuwa imeandaa moja ya mashindano ya vijana. Lakini kwa kuwa suala hili liko katika mazingira maalumu (exceptional circumstances) tunaamini CAF watafikiria ombi letu kwa msingi huo.
Awali Libya ilipewa uenyeji wa fainali hizo 2015, lakini zikahamishiwa Afrika Kusini kutokana na sababu za kiusalama. Hivyo, Libya ikapewa fainali za 2017 ambapo sasa imejitoa yenyewe kuandaa fainali hizo.
RUSHWA NA KUPANGA MATOKEO
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeamua kuanzia sasa adhabu kwa watu wanaotoa rushwa au kupanga matokeo katika mpira wa miguu kuwa ni kufungiwa maisha kujishughulisha na mchezo huo.
0 Comments