Jose Mourinho anasema Fernando Torres ni sehemu ya mipango yake katika klabu ya Chelsea na kwamba
mshambuliaji huyo hajamwambia kwamba anataka kuondoka.
Torres amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa msimu huu, na AC Milan hivi karibuni wameonyesha nia ya mshambuliaji huyo baada Mario Balotelli kujiunga na Liverpool.
Lakini Mourinho anasema anamuhitaji mchezaji huyo wa miaka 30 kucheza na kuwa sehemu katika kikosi chao kwa ajili ya kupata vikombe msimu huu.
"tuko wazi ni kwamba tunahitaji washambuliaji watatu msimu huu," alisema Mourinho. "Yeye ni mmoja wao".
"Namuhitaji mtu kama yeye,nahitaji mchezaji kama yeye. Kama yeye anataka kuondoka ni kitu ambacho hakuniambia mimi. Kwa sasa yeye ni mchezaji wetu, hakuna kitu zaidi ya hicho".
"Kama yeye anataka kuondoka Naamini ni kwa sababu yeye anataka kujaribu maisha mapya, klabu mpya, ligi mpya Kama yeye anataka kuondoka Naamini ni kujaribu na kuwa na furaha kuliko aliyokuwa nayo miaka michache iliyopita". .alisema Jose Mourinho .
0 Comments