UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union
ya Tanga umemfungia aliyekuwa beki wa kushoto Abdi Banda kucheza mpira wa miguu
ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kukosa nidhamu na
kusaini mikataba katika vilabu viwili tofauti.
Adhabu hiyo itahusisha
kutokucheza mechi zozote ikiwemo zile za kirafiki kutokana na kukiuka
makubaliano aliyoingia na klabu hiyo ya Coastal Union wakati aliposajiliwa.
Akitoa taarifa hiyo kwa
waandishi wa habari leo,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa
uongozi umeamua kumpa adhabu hiyo kwa
kukosa nidhamu pale aliposaini mkataba mwengine na timu ya Simba SC ya Dar es
Salaam wakati akijua tayari ana mkataba wa miaka mitatu na timu ya Coastal
Union.
El Siagi alisema kuwa
mchezaji huyo alikuwa amebakiza miaka miwili kucheza timu ya Coastal Union na
hivi sasa yupo katika mikataba miwili kwa timu mbili tofauti ambazo zinashiriki
ligi moja.
“Ki ukweli hali hii hatuweza kuivumilia ndio
maana tumeamua kuchukua hatua hiyo kali ili iweze kuwa fundisho kwa wachezaji
wengine wenye tabia kama hii “Alisema Katibu El Siagi.
Alisema kuwa kutokana na hali
hiyo mchezaji huyo atakuwa amevunja sheria na kanuni za mchezo wa mpira wa
miguu hapa nchini na kulitaka shirikisho la soka kutoa ushirikiano katika
maamuzi hayo.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments