Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi mpya
wa Mashindano kuanzia Septemba 1 mwaka huu.
Kabla ya uteuzi huo, Wambura alikuwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF kuanzia Januari 1, 2011. Nafasi hiyo sasa iko wazi na itajazwa baadaye na Kamati ya Utendaji.
Kamati ya Utendaji ya TFF inamtakia kila la kheri Wambura katika wadhifa wake huo mpya.
0 Comments