Ticker

6/recent/ticker-posts

TAIFA STARS NA MSUMBIJI YAINGIZA MILIONI 158/-

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.JUL.22,2014 SAA 09:17 ALASIRI

Picha na blog ya francis dande
Shirikisho la soka nchini Tanzania limetangaza mapato yaliyopatikana katika mechi ya timu ya taifa ya
Tanzania(Taifa stars) na timu ya Msumbiji (Mambaz) katika mechi iliyomalizika kwa sare ya 2-2 iliyochezwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa jijini dar es salaam.

Akitangaza mapato hayo Ofisa wa Habari wa Tff Boniface Wambura amesema mechi hiyo imeingiza shilingi Milioni Mia moja hamsini na nane,Laki tatu na elfu hamsini (158,350,000 ) kutokana na washabiki 19,684 walioingia kwa kiingilio cha sh. 7,000 na sh. 30,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 24,155,084.75, gharama za tiketi (MaxMalipo) sh. 19,684,000, gharama za mchezo sh. 22,902,183, uwanja sh. 11,451,092, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 5,725,546 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 74,432,095.

Tff imewashukuru mashabiki waliojitokeza kushuhudia mechi hiyo kwa ajili ya kuisapoti timu yao ya taifa.

Taifa stars inatarajiwa kuingia kambini mjini Tukuyu mkoani mbeya siku ya Alhamisi,ambapo itakuwa na kambi ya wiki moja,na July 31 timu itaondoka kwenda Johanesbag Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo siku mmoja kabla ya Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco ambapo itakayofanyika wikiendi ya Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.

ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments