Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.JUL.18,2014 SAA 04:06 USIKU
Shirikisho la soka Duniani FIFA imeifungulia nchi ya Nigeria kwa kufuta adhabu ya kufupiwa marufuku kushiriki
mashindano yeyote ya kandanda yanayoandaliwa na shirikisho hilo.
FIFA iliifungia Nigeria baada ya maafisa wa serikali kuwaondoa wasimamizi wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF afisini, lakini serikali ya nchi hiyo ikanyoosha mikono juu kwa kuwarudisha madarakani viongozi wa shirikisho la soka nchini humo.
Marufuku hiyo ilikuwa inamaanisha hakuna klabu yeyoye ya soka nchini Nigeria ambayo inaweza kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa.
Hatua ya FIFA kuifungulia Nigeria,imekuwa habari njema kwa timu ya taifa ya Super Eaglets ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 ambayo inapaswa kushiriki mchuano wa kombe la dunia.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments