Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA/KIKAPU:TIMU YA WANAUME YA DAR YASHINDWA KUTAMBA KWA TIMU YA CAIRO,FAINALI HAPO KESHO NI KATI YA

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 06,2014 SAA 04:22 USIKU
Mashindano ya Mpira wa Kikapu kwa Majiji ya Afrika Mashariki na Kati, yaliyoanza Siku ya tarehe 6
May,yameendelea hii leo kwa michezo mitatu kupikwa katika uwanja wa ndani wa Taifa.




Mchezo wa kwanza ulikuwa ni wa wanawake ambao ulikutanisha timu ya jiji la Kampala na timu ya jiji la Dar es salaam,ambapo katika mchezo huo timu ya jiji la Kampala iliibuka na ushindi wa alama 64 dhidi ya alama 52 za jiji la Dar es salaam.

Mchezo wa nusu fainali ya kwanza kwa wanaume ilikutanisha timu ya  Gorowe na timu ya Citizen ambapo timu ya Gorowe imeibuka na ushindi wa alama 81 dhidi ya alama 54 .





Nusu fainali ya pili ilikuwa ni kati ya timu ya jiji la Cairo na timu ya jiji la Dar es salaam,ambapo wenyeji watanzania wameshindwa kubakisha ubingwa wa mashindano hayo nyumbani baada ya kukubali kupata alama 56 dhidi ya alama 84 ambazo wamepata jiji la Cairo.





Kwa maana hiyo fainali kwa wanaume itakutanisha jiji la Gorowe kutoka Somalia na jiji la Cairo kutoka misri hapo kesho.


Post a Comment

0 Comments