Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 06,2014 SAA 09:24 USIKU
Mashindano ya Mpira wa Kikapu kwa Majiji ya Afrika Mashariki na Kati yaliyoanza Siku ya tarehe 6 May,yamemalizika jana 10 May 2014 katika uwanja wa
ndani wa Taifa.
 |
Kikosi cha jiji la Gorowe kutoka Somalia |
 |
Kikosi cha Jiji la Cairo kutoka Misri |
Katika michuano hiyo iliyohusisha timu za majiji takribani 11 kutoka Afrika mashariki,yameleta hamasa kubwa kwa wapenzi wa mchezo huo hapa nchini, kwani kumukuwa na wingi wa watu waliojitokeza kushuhudia michuano hiyo huo,ambayo iliyodhamini na Azam TV
Fainali ya kwanza ilikuwa ni ya wanawakea iliyokutanisha jiji la Kampala na jiji la Nairobi,fainali hiyo ilikuwa ni ushindani mkubwa kwani mchezo ulimalizika kwa kupishana alama moja tu, kwa jiji la Nairobi kuibuka na ushindi wa alama 59 dhidi ya alama 58.
 |
Wanawake: Kampala wakipambana na Nairobi |
 |
Furaha ya ushindi:Wachezaji wa Nairobi wakifurahia ushindi |
 |
Wachezaji wa Nairobi wakicheza baada ya ushindi |
Fainali ya pili ilikuwa ni ya wanaume,jiji la Gorowe kutoka Somalia ilikutana na jiji la Cairo kutoka Misri,vidume hivyo vilioneshana ubabe kweli kweli ,mwanzo mzuri walionesha Gorowe kwa kuongoza katika kota ya kwanza baada ya kupata alama 27 dhidi ya 19 za Cairo,lakini mambo yakazaanza kuonekana mabaya Baada ya kuingia katika kota ya pili kwani Cairo walizinduka na kuongoza katika kila kota iliyofuata.
 |
Timu ya Cairo kutoka Misri |
 |
Wachezaji wa Gorowe wakipambana na wachezaji wa timu ya Cairo |
 |
Kocha wa timu ya Cairo akitoa maelekezo |
 |
Matokeo ya mwisho |
Kota ya pili Cairo waliibuka na alama 26 dhidi ya 22,kota ya tatu wakapata alama 23 dhidi ya alama 12,na mwisho wa mchezo Cairo wakapata alama 20 dhidi ya 13,na matokeo kwa ujumla Timu ya Cairo kutoka Misri ikaibuka na ushindi wa jumla ya alama 88 dhidi ya alama 74 za timu ya Gorowe kutoka Somalia.
 |
Wachezaji Cairo wakifurahia ushindi |
 |
Furaha ya ushindi |
 |
Mgeni rasmi( Katikati) Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa |
Wawakilishi wa Tanzania timu ya wanaume ya Dar es salaam walipata nafasi ya tatu katika mashindano hayo baada ya kuwachapa timu ya Citizen kwa alama 55 dhidi ya alama 49.
0 Comments