Ticker

6/recent/ticker-posts

KESI YA OSCAR PISTORIUS ITACHELEWA TENA KWA SABABU HII

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 15,2014 SAA 12:52 USIKU
Oscar Pistorius: To undergo psychiatric tests
Kesi ya Oscar Pistorius itachelewa kwa ajili ya kuruhusu
mwanamichezo huyo wa Olimpiki kufanyiwa vipimo vya akili.

mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Jumanne ijayo,ili utaratibu maalum ulitolewa na hakimu kwa ajili ya tathmini kuchukua nafasi yake.

Pistorius hatakaa katika kitengo cha akili, lakini itakuwa akitibiwa kama " mgonjwa wa nje."

Mnamo Jumatatu, Daktari Bingwa wa akili, aliambia Mahakama kuwa Bwana Pistorius anaugua maradhi yanayaohusiana na kuhangaika.

Hakuna maelezo ya muda mrefu waliyopewa ya jinsi tathmini hiyo itakavyokuwa, ingawa inaeleweka kuwa inaweza kuchukua muda mrefu kama siku 30.

Uamuzi wa Jaji Thokozile Masipa  ulifuatia ombi la tathmini ya akili kutoka kwa mwendesha mashitaka mkuu, Gerrie Nel siku ya Jumanne.

Mwanariadha huyo hivi sasa yuko nje kwa dhamana na alikiri kumuuwa mpenzi wake Reeva  Steenkamp lakini amekanusha kwamba alifanya hivyo kwa kukusudia akisema kwamba alimpiga risasi kupitia mlango wa choo  cha nyumba yake uliokuwa umefungwa kwa kumdhania kuwa ni mwizi,katika nyumba yake iliyoko Pretoria alfajiri ya tarehe 14 mwezi wa Februari mwaka 2013 .

Post a Comment

0 Comments