Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 06,2014 SAA 11:11 ALFAJIRI
Ryan Giggs ameahidi kwamba 'wakati mzuri' unarudi kwa timu ya Manchester United baada ya kucheza mechi yake ya
mwisho akiwa nyumbani na klabu hiyo ya Old Trafford.
Mkongwe huyo ambaye aliteuliwa kama meneja wa mpito kufuatia kufungishiwa virago kwa David Moyes mwezi uliopita,alijiweka mwenyewe kwenye benchi la wachezaji wa akiba,katika mchezo dhidi yao na Hull City.
Giggs ambaye yeye mwenyewe alichukuwa maamuzi ya kuchukuwa nafasi ya kinda Tom Lawrence dakika 20 za mwisho wa mchezo ambao waliibuka na ushindi wa 3-1 .
Mashetani hao wekundu ambao wamepigwa mara saba katika ligi mbele ya mashabiki wao wenyewe msimu huu, pia walitolewa katika mashindano ya Kombe la FA na Capital One Cup na mtiririko wa matokeo mabaya kwa timu hiyo ikiwa nyumbani.
Matokeo hayo ndiyo yalimuondoa Moyes aliletwa ili amrithi Sir Alex Ferguson, na kupewa Giggs kwa muda jukumu huku kukisubiliwa kwa kocha Louis van Gaal ambaye atachukua kazi kwa muda mrefu.
Giggs aliwaambia mashabiki waliojazana katika uwanja wa Old Trafford baada ya mechi: "Tunajua imekuwa vigumu msimu huu na zaidi ya miaka tumekuwa tukiharibiwa mafanikio tuliyo nayo".
"Msaada wenu mwaka huu haujabadilika, daima mnaiunga mkono timu na wafanyakazi, nina uhakika katika miaka ijayo tuleta mafanikio zaidi".
"Ningependa tu kusema, endeleeni kutusaidia, tutaona mafanikio kidogo ya baadaye"
"Tutaendelea kusimama, sisi daima tunawapa vijana nafasi na kujaribu kucheza mchezo wa kuvutia "
"Wakati mwingine hatuwezi kushinda, lakini tunafanya kila kitu. Kuweza kusaidia na wakati mzuri unakuja tena hivi karibuni."alisema Giggs akiwaambia mashabiki baada ya mchezo.
0 Comments