Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 12,2014 SAA 11:46 JIONI
Polisi nchini Ghana wameanzisha uchunguzi wa kifo cha mwamuzi msaidizi wa mpira wa miguu,
ambaye ameripotiwa kudhalilishwa
kwa kupigwa vibaya, baada ya kutoa maamuzi ya utata
katika mechi ya ligi ya ndani nchini humo, msemaji wa polisi nchini humo amesema hii leo Jumatano.
Kwame
Andoh Kyei, ambaye alifariki siku ya Ijumaa, alikuwa mwamuzi msaidizi
katika mechi ya daraja la pili, iliyopingwa katika mji wa magharibi wa Bordie Machi 2.
Msemaji
wa chama cha mpira cha Ghana, Ibrahim Sannie Daara alisema Kyei ilidhalilishwa baada ya uamuzi wa utata,lakini hakuwai mara moja
kutafuta matibabu.
Olivia
Adiku, msemaji wa polisi katika mkoa wa magharibi, alisema wapelelezi walikuwa
wakisubiri maelezo ya uchunguzi ambayo yanaweza kuja wiki hii.
Ilikuwa wazi kuwa mwamuzi Kyei alikufa kutokana na majeraha endelevu wakati wa mechi, aliongeza Olivia
Adiku,ambaye ni msemaji wa polisi katika mkoa wa magharibi.
"Kwa sasa, hatuwezi kusema kama ni timu iliyokuwa nyumbani ambao walimshambulia au timu ya ugenini," Daara aliiambia AFP.
Polisi
ni kawaida hutoa usalama katika mechi maalumu katika
mkoa wa magharibi lakini hawakuwepo Machi 2 kwa sababu klabu "hawakuweza
kuomba kibali kwa ajili ya usalama fulani", alinukuliwa Adiku akisema.
Alisema kutokea kwa vurugu zinazohusisha mpira ni nadra sana katika eneo hilo.

0 Comments