Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 12,2014 SAA 10:05 ALASIRI
Meneja wa AC Milan Clarence Seedorf amesema kuwa "amehudhuniswa" kwa timu yake kutoka katika Ligi ya Mabingwa
Ulaya.
Timu hiyo ya Italia, ilibugizwa kwa jumla ya mabao 5-1 dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wao wa mwisho katika hatua ya 16 bora.
Milan baada
ya kupoteza mechi ya kwanza kwa mabao 1-0 mwezi uliopita,Rossoneri (The Red and Blacks) pia wakachapwa mabao 4-1 katika uwanja wa Vicente Calderon huko mjini Madrid siku ya jana
Jumanne.
"Tumekata tamaa, bila shaka, kwamba tumetolewa nje ya Ligi ya Mabingwa," aliiambia Sky Sports 1.
"Atletico walianza vizuri na kufunga bao la mapema. Tulikuwa na majibu mazuri, lakini tulikubali tena kufungwa dakika tano kabla ya mapumziko, na kisaikolojia alifanya kuwa vigumu kupona katika kipindi cha pili."
0 Comments