Na,Falysiah Lyimo,IMEWEKWA March. 16,2014 SAA 12:20 JIONI
Chama cha wanawake vijana cha kikristo(YWCA) kimewakumbuka na kuwatembelea wazee wasiojiweza na kutoa
misaada mbalimbali ikiwemo malazi,chakula,pamoja na mahitaji mengine katika kitoo cha kulea wazee wasiojiweza kilichopo chini ya kanisa katoliki jimbo kuu la Dar es salaam Msimbazi Center.| sister Wilibroda Mangwangwe |
Akipokea vitu hivyo kwa niaba ya wazee hao sister Wilibroda Mangwangwe wa shirika la masister wa upendo mtakatifu Fransisko jimbo la Mahenge,ameweza kueleza juu ya shughuli wanazozifanya kwa ajili ya kulea wazee hao pamoja na kueleza changamoto mbalimbali wanazopata pindi wanapotoa huduma kwa wazee hao hususani kuwashukuru YWCA kwa kuguswa katika kuwakumbuka wazee wasiojiweza.
| Sister Wilibroda Mangwangwe akiwa na katibu wa tawi la Dar es salaam Bi Manka Kimaro (kulia) |
Kwa upande wake katibu wa tawi la Dar es salaam Bi Manka Kimaro ameweza kueleza lengo kutoa msaada huo pamoja na kuitaka jamii kujitoa na kuwatembelea wazee hao kwa kuwasaidia pamoja na kuwatia moyo..
Naye mmoja wa wanachama wa YWCA bi. Jastina Katunzi amesema kuwa ni vyema jamii ikayakumbuka makundi mbalimbali yanayohitaji masaada katika jamii katika kipindi hiki cha kwaresma kwani ni mojawapo ya sadaka yoko mbele ya mungu.
0 Comments