Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA March. 05,2014 SAA 07:05 USIKU
Kufuatia Taarifa kutoka Cairo Misri ya kuwaonya mashabiki mashabiki wa Timu ya Aly Ahly kutoingia uwanjani uwanjani katika uwanja wa Cairo kuhudhulia mechi ya raundi ya pili ya
michuano ya Clabu bingwa Afrika kati ya timu ya Aly Ahly ya nchini humo dhidi ya timu ya Yanga ya Tanzania .
Ikiwa ni takribani siku tano kabla
ya kufanyika mchezo wenyewe wenyeji Al Ahly wameshindwa kuweka wazi ni
uwanja gani utakaotumika kwa ajili ya mchezo huo huku Meneja wa klabu
hiyo Abdoulazi akisema huenda mchezo ukachezwa jijini Cairo au
Alexandria na kusema majibu kabili yatapatikana siku ya jumatano mchana.
Wenyeji
wameiandalia timu ya Young Africans kufikia katika Hoteli ya Baron
iliyopo maneneo ya Uwanja wa michezo wa kimataifa Cairo huku pia
wakiipangia timu kufanya mazoezi katika uwanja wao uliopo eneno la Nasri
City.
Mchezo wa jumapili unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Arab
Contractors uliopo jijini Cairo huku mechi hiyo ikichezwa bila ya
mashabiki kufuatia Serikali ya Misri kuzuia mashabiki wa soka kutokana
na mashabiki hao kufanya vurugu katika mchezo wa Fainal ya Super Cup
dhidi ya CS Sfaxien na kupelekea askari kadhaa kujeruhiwa.
Shirikisho la soka hapa nchini limefanya maamuzi.
Msikilize ofisa habari na mawasiliano wa tff Boniface Wambura Mgoyo akieleza walichokifanya.

0 Comments