Ticker

6/recent/ticker-posts

ROBBEN,MACHO YOTE KATIKA MKATABA MPYA NA BAYERN MUNICH

 Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 8,2014 SAA 08:16 USIKU

Nyota wa Uholanzi Arjen Robben amesema kuwa anatarajia kutia saini mkataba mpya na klabu ya Bayern Munich hivi karibuni, na
amekiri kuwa yeye anaangalia maisha yake ya baadaye ya mpira wa miguu.
  
Robben  mkataba wake unamalizika Juni mwaka 2015 na ana matumaini ya kuongeza tena miaka miwili.

Robben anasema anatarajia kutia saini mkataba mpya wakati mchache kutoka sasa ila "maelezo kidogo" yamekuwa yakikamilika.

 "pengine yataamuliwa baada ya mazungumzo mengine," Robben aliiambia Bild. "Lengo ni hilo, kutoka pande zote mbili, kutanua, lakini hakuna tatizo na mshahara,kwani nimesoma mahali fulani, - huyu ni ng'ombe***".

Robben imekuwa akitiliwa mashaka kutokana na makali yake katika kazi yake na tangu kujiunga na Bayern mwaka 2009, amekuwa majeruhi mara 25, lakini bado ameweza kufunga mabao 52, na kusaidia mara 34, katika mechi 92 za Bundeslig,pia aliongoza ushindi katika fainali ya msimu uliopita ya Ligi ya Mabingwa .

Post a Comment

0 Comments