Ticker

6/recent/ticker-posts

MICHAEL LAUDRUP KUCHUKUA HATUA ZA KISHERIA BAADA YA KUTIMULIWA KATIKA KLABU YA SWANSEA CITY

  Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 6,2014 SAA 11:40 JIONI

Michael Laudrup amathibitisha kuwa atachukua hatua za kisheria baada ya kufukuzwa kazi ya umeneja wa kikosi cha Swansea City
siku ya Jumanne. 

Kocha huyo raia wa Denmark ambaye aliongoza Swans katika ushindi wa kombe la Ligi mwaka jana, anasema hajaruhusiwa kurudi tena katika uwanja wa mazoezi kwa ajili ya kuwaaga na kusema kwa Kheri kwa wafanyakazi na wachezaji.

Katika taarifa kupitia kwa mameneja wa chama kinachosimamia Ligi(LMA), Laudrup anadai kuwa bado anasubiri kusikia sababu ya kufukuzwa kazi katika timu ya Swansea City.

"Mimi , bila shaka, nitachukua  hatua za kisheria," alisema Laudrup.
 
"LMA tayari imeandika barua kwa klabu kuuliza kwa maelezo sahihi, kwa nini nilikuwa hapo na kufukuzwa kazi".
 

Post a Comment

0 Comments