Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 6,2014 SAA 12:35 ASUBUHI
Robert Lewandowski amefafanua malengo yake ya mwisho akiwa katika kikosi cha Borussia Dortmund kuwa anataka kushinda
kikombe cha mwisho kabla ya kuhamia rasmi katika klabu ya Bayern Munich msimu huu.
kikombe cha mwisho kabla ya kuhamia rasmi katika klabu ya Bayern Munich msimu huu.
BVB sasa wako nyuma kwa alama 17 kwa Bayern ambao ndio viongozi wa ligi hiyo ya Bundesliga na wana uwezekano wa kuwa mabingwa wa ligi hiyo kwa muda huu.
Hata
hivyo, Dortmund bado wana nafasi ya kushinda kumbe kuu kama
watafanikiwa raundi ya 16 ya Ligi ya Mabingwa, ambapo wao watakutana na Zenit St
Petersburg, na DFB Pokal katika robo fainali, ambayo watawasubiri Eintract Frankfurt.
"Lengo langu bado ni kuondoka Borussia Dortmund na kikombe msimu huu wa majira ya joto," Lewandowski alinukuliwa akisema na Sport Bild.
"Lakini sisi sote tunajua tunatakiwa kuboresha. Bila shaka, tulikuwa na wachezaji wengi majeruhi, lakini wote walipoona na timu inatakiwa kushinda kila mchezo".
"Watu wengi wanadai kwamba mimi sina nia tena ya kucheza katika timu ya Dortmund, lakini mimi
ninaonyesha kuwa bado nina nia ya kucheza kwa BVB. Nataka kuwapa
mashabiki zawadi nzuri ya kuwaaga."
Lewandowski ametikisa nyavu mara 11 katika mechi 19 za Bundesliga alizoshiriki msimu huu,
lakini bado hajafunga tangu kutangaza uhamisho wake kwenda Bayern.

0 Comments