Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 13,2014 SAA 03:31 USIKU
![]() |
Rais wa Tff akimkabizi Jezi muwakilishi wa Dar es salaam |
Shirikisho la soka nchini Tff leo limeweka bayana mikakati yao ya kuboresha timu ya Taifa kwa kuanzisha Ligi ya mikoa yote
Tanzania ili kupata wachezaji 60 na baadaye kuchujwa na kupata wachezaji 30 ambao wataweka kambi wilayani Rungwe mkoani Mbeya mwezi March.![]() |
Rais wa Tff akimkabizi Jezi muwakilishi wa Lindi |
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Rais wa Tff Jamal Malinzi amesema kuwa,ana uhakika mpango huo utasaidia Tanzania kuweza kucheza michuano ya AFCON mwakani,Malinzi amesema kuwa Ligi itachezwa katika Zone husika za Tff ambapo mpaka sasa vifaa pamoja na pesa tayari zimetumwa katika mikoa yote.Na wachezaji wa timu ya Taifa wataungana na hao 30 ambao wamechaguliwa katika ligi za mikoa,mara baada ya Ligi kuu kumalizika Mwezi wa 4.
![]() |
Jamali Malinzi (katikati) kilia ni Raisi wa chama cha mpira Zanzibar Ravia Idarous Faina |
"Ili kuimarisha Kikosi chetu cha Taifa, TFF ilianza kwa kuandaa kikao cha walimu wa mpira na baadhi ya wachezaji wa zamani huko Zanzibar mwezi Desemba mwaka jana na mapendekezo yalitolewa tulifanyia kazi na mwezi Janauari tuliitisha kikao na makatibu wote wa mkoa kujadili utaratibu wa kuimarisha kikosi chetu cha taifa.Kwa kuwa hatuna mashindano ya kombe la taifa ambalo kwa miaka mingi limekuwa ndilo chimbuko la kuibua wachezaji wa timu ya taifa tumeonelea njia mbadala iwe ni kufanya mashindano madogo ya kukutanisha timu mbili za mikoa ambazo zitacheza nyumbani na ugenini kati ya tarehe 22 Februari na 05 Marchi 2015.kila mechi itahudhuriwa na waibua vipaji watano na itarekodiwa.Waibua vipaji walioteuliwa kwa kazi hii ni pamoja na walimu wa mpira,wadau wazoefu kwa kuendeleza vipaji pamoja na wachezaji wa Timu wastaafu.Orodha yao itaanbatanishwa hapa.Kila mchezo utarekodiwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye"
0 Comments