IMEWEKWA FEB. 13,2014 SAA 10:42 JIONI
Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Uganda na timu ya Young Africans
leo ameruhiswa ramsi kuanza kuitumikia timu yake katika
michezo ya Ligi
Kuu na Mashindano ya klabu Bingwa Barani Afrika kufuatia shirikisho la
soka nchini TFF kuiandikia barua klabu ya Young Africans.
Okwi ambaye alisajiliw aa Young Africans mwishoni mwa mwaka jana na
kucheza michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya, alisimamishwa na
Shirikisho la Soka la Nchini TFF wakati wakisubiria kupata udhibitisho
wa usajili wake kutoka FIFA.
Mara baada ya barua hiyo, Okwi
anatarajiwa kuungana na wenzake mwishoni mwa wiki mara timu itakaporejea
kutoka Visiwa vya Comoro na ataanza kuonekana katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom dhidi ya Ruvu Shooting siku ya jumamosi Februari 22 mwaka
huu.
Uongozi wa Young Africans
unawashukuru wanachama, wapenzi na wadau kwa ujumla kwa kuwa wavumilivu
wakati wa suala na hili na hatimaye limepatiwa ufumbuzi.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz

0 Comments