Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA FEB. 14,2014 SAA 06:01 USIKU
David
Moyes anaona timu yake ya Manchester United bado iko katika vita kwa ajili ya kugombea nafasi nne za juu katika ligi kuu
ya Barclays baada ya kutoka sare ya bila kufungana na timu ya Arsenal.
Nafasi walikuwa nayo katika Ligi kuu,ambayo imeshindwa kuwapandisha, matokeo yake imezidi kuibakisha kileleni Chelsea katika msimamo.
United
ingeweza pia kuondoka London kaskazini na ushindi kama si kipaji
cha kuokoa mikwaju kutoka Wojciech Szczesny, ambaye alisukuma nje makombola kutoka kwa Robin van
Persie .
United, wametolewa nje ya Kombe la FA katika raundi ya tatu,na sasa watakuwa na
mapumziko ya mazoezi huko Dubai kabla ya kuanza kwa hatua ya Ligi Kuu kwa kupambana na
Crystal Palace Februari 22.
"Ninachoweza kufanya -na kuendelea kusema - ni sisi kujaribu na kushinda mchezo ujao na kujiweka juu," alisema Moyes.
"Kama
kuna klabu moja katika historia ambao wamekuwa na nguvu ya kushinda
michezo katika nusu ya pili ya msimu na kuweza kuleta pressure kwa timu za
juu, ni Manchester United.Tutaendelea kujaribu na kufanya hivyo na
kufanya kazi yetu."
"Tunaweza kufanya kazi yetu bora, tunaweza,tunataka kucheza vizuri,hatuwezi kusumbua timu nyingine,tunaweza tu kuleta pressure na
kushinda michezo yetu."
Moyes aliongeza: "Naamini hamu bado ipo katika kikosi".
0 Comments