Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA JANUARI 17,2014 SAA 12:12 JIONI
Shrikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Somalia
kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa
Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na
Komorozine Sports ya Comoro.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya mchujo itafanyika jijini Dar es Salaam kati
ya Februari 7 na 9 mwaka huu wakati ile ya marudiano itachezwa kisiwani
Comoro kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Mwamuzi
wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi wakati wasaidizi wake ni Hamza Hagi
Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir Olab Arab. Kamishna wa mechi hiyo
atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.
Timu
ambazo zimeingia moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa ni Coton Sport ya Cameroon, El Ahly (Misri), TP Mazembe
(Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Hilal (Sudan), Club Sportif
Sfaxien (Tunisia) na Esperance (Tunisia)
Nayo
mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kati ya Azam ya Tanzania na
Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayofanyika Dar es Salaam kati ya
Februari 7 na 9 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Sudan.
Waamuzi
hao ni Mutaz Abdelbasit Khairalla atakayepuliza filimbi, Waleed Ahmed
Ali, Aarif Hasab Elton na El Fatih Wadeed Khaleel. Kamishna wa mechi
hiyo ni Hassan Mohamed Mohamed kutoka Somalia. Mechi ya marudiano
itachezwa Msumbiji kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Timu
zilizotinga moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo ni
Asec Mimosas ya Ivory Coast, Ismailia (Misri), Wadi Degla (Misri),
Djoliba (Mali), MAS (Morocco), Bayelsa United (Nigeria), El Ahly Shandy
(Sudan), E.S.S. (Tunisia), C.A.B. (Tunisia) na Zesco United (Zambia).
0 Comments