Ticker

6/recent/ticker-posts

MOYES AKIRI KUWASHINDWA SUNDELAND

Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 23,2014 SAA 12:12 ASUBUHI

Meneja wa Manchester United David Moyes amekiri kwamba timu yake haikustahili kushinda katika mchezo wa mwisho wa kombe la
Capital One baada ya kufungwa na timu ya Sunderland katika uwanja wa Old Trafford katika mechi ya pili ya nusu fainali.

United ililazimika kuyaaga mashindano hayo baada ya kushindwa kupitia kwa mikwaju ya penalti na Sunderland.

Baada ya muda wa kawaidia United ilikuwa ikiongoza kwa goli moja kwa bila lililofungwa na Jonny Evans dakika ya 37, lakini kama unakumbuka United walipoteza mechi ya awali kwa magoli mawili kwa moja, na hatimaye mechi hiyo ilibidi kuongezwa dakika thelathini za ziada.

Katika muda huo wa ziada Sunderland nusura ifuzu moja kwa moja baada ya kupata bao kupitia kwa mchezaji wao Phillip Bardsley,lakini sherehe hizo zilikatizwa baada ya dakika moja pale United waliposawazisha kupitia kwa nyota wake Chicharito, na hivyo kufanya timu hizo mbili kutoshana nguvu ya jumla ya magoli matatu kwa matatu bada ya dakika mia moja na Ishirini.

Mechi hiyo iliamuliwa kupitia mikwaju ya penalti na kwa mara ya kwanza, makipa wa timu hizo mbili waliokoa mikwaju kadhaa.
Kwa ujumla Mikwaju minne iliokolewa na mitatu kupigwa nje na hivyo Sunderland kujikatia tikiti ya fainali ambapo watakutana na Manchester City kwa jimla ya penalti mbili kwa moja.

Mara baada ya mchezo kumalizika Moyes alikataa kuongelea swala la mchezaji wa Chelsea Juan Mata na badala yake kuongelea swala la mchezo wenyewe.

"Bila shaka Sunderland, wao walicheza vizuri na sisi hatukucheza vizuri usiku huu," aliiambia Sky Sports News.

"kipindi matokeo yakisomeka (kwa pamoja jumla ya mabao  2-2) tulidhani sisi wenyewe tunapita,tumerudi nyuma na sisi tulikuwa na nafasi katika penalti lakini kwa ujumla sisi hatukucheza vizuri usiku wa leo".

"michezo mingi ya msimu huu tunacheza vizuri,lakini kiukweli Sisi atukustahili kitu chochote usiku wa leo kwa jinsi tulivyocheza."
"Lakini Sunderland walicheza vizuri na mimi sina tatizo na wao kupitia, wao walistahili ." 

Moyes alipinga kuwa makosa makubwa yalifanywa na kipa David De Gea, baada ya kuruhusu goli la BARDSLEY.

"David imekuwa mzuri msimu huu lakini kila mtu hufanya makosa," aliongeza Mscotsman huyo. 

Moyes pia alikiri kuwa alisikitika kwa timu yake kukosa penalti nne kati ya penalti tano katika kipindi cha kupigiana penalti. 

Fainali ya kombe hilo itachezwa tarehe mbili mwezi Machi mwaka huu katika uwanja wa Wembley. 

Wakati huo huo Ombi la Manchster United la kutaka kumsajili nyota wa Chelsea Juan Matata imekubalika.
Ripoti zinasema United imetumia takriban kitita cha pauni milioni 37 kumsajili mcheza kiungo huyo wa Chelsea.

Mata mwenye umri wa miaka 25, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu baadaye hii leo, kabla ya kukamilisha usajili huo.

Mchezaji huyo kutoka Uhispania anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu hiyo iliyo na makao yake katika uwanja wa Old Trafford.

Mata ambaye aliichezea Chelsea, mechi 32, aliwaaga wachezaji wenzake na wakufunzi wa Chelsea katika uwanja wao wa mazoezi wa Cobham siku ya Jumatano.

 

Post a Comment

0 Comments