Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA JANUARI 12,2014 SAA 01:21 USIKU
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amezindua
programu ya kutoa elimu ya kupambana
na matumizi ya dawa za kulevya kwa
vijana iitwayo Ishi Huru.
Programu
hiyo iliyozimduliwa jana (Januari 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam
iko chini ya taasisi ya Africa Inside Out inayoongozwa na Rebecca Young
wakati washirika (partners) ni TFF na kampuni ya Rhino Resources ya
Marekani.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akizungumza kwenye uzinduzi wa programu ya Ishi Huru jijini Dar es Salaam. |
Rais
Malinzi amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamekuwa
yakiongezeka, hivyo kuwa kikwazo kwa maendeleo ya vijana ambapo
ameipongeza Africa Inside Out kwa programu hiyo kwa vile itazuia vijana
wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo.
“Moja
athari kubwa za matumizi ya dawa za kulevya ni kupata maambukizi ya
virusi vya Ukimwi kutokana na kuchangia sindano za kujidunga dawa hizo.
“TFF
tutatoa ushirikiano wa kutosha katika programu hii. Lakini pia
tutaingiza Ishi Huru katika programu zetu za mpira wa miguu kwa vijana.
Tutahamasisha jamii katika kupambana na dawa za kulevya,” amesema.
Katika
uzinduzi huo, pia Rais Malinzi alizundua semina ya waelimishaji na
kuwaeleza kuwa wamepata fursa hiyo kwa vile ni vijana wanaojituma, hivyo
watafikisha vizuri ujumbe wa Ishi Huru katika shule na vituo vya vijana
nchini.
0 Comments