Ticker

6/recent/ticker-posts

MALINZI KUTEMBELEA KITUO CHA ALLIANCE

 Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA JANUARI 12,2014 SAA 091:21 USIKU

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atafanya ziara ya siku moja kutembelea kituo cha
mpira wa miguu wa vijana cha Alliance cha jijini Mwanza.

Lengo la ziara hiyo ni kuangalia jinsi Alliance inayoendesha shughuli zake ili Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liweze kushirikiana na kituo hicho kwa karibu.

Rais Malinzi katika ziara hiyo atakayoifanya keshokutwa (Januari 15 mwaka huu) atafuatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu kwa Vijana, Ayoub Nyenzi na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ramadhan Nassib.

Alliance inatarajia kufanya mashindano yatakayoshirikisha vituo vyote vya kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana (academy) wiki ya tatu ya Februari mwaka huu jijini Mwanza.

Mashindano hayo yatashirikisha timu za umri wa miaka 13, 15 na 17 ambapo Alliance itagharamia malazi, chakula na usafiri wakati timu hizo zikiwa jijini Mwanza.

YAHYA KUFUNGA SEMINA YA WAAMUZI, MAKAMISHNA
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Hamad Yahya atakuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa semina ya waamuzi na makamisha.

Semina hiyo ya siku mbili itafungwa kesho (Januari 14 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi zaidi ya 100 na makamishna 50 wanashiriki katika semina hiyo. Makamishna hao ni baadhi ya wale wanaosimamia mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Kwa upande wa waamuzi ni wale wa daraja la kwanza (class one) ambao ndiyo wanaochezesha mechi za VPL na FDL.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kuandaa semina nyingine baadaye mwaka huu kwa makamishna wapya wanaotaka kusimamia mechi za VPL na zile za FDL.

Post a Comment

0 Comments