Ticker

6/recent/ticker-posts

KIKAPU:ABC NDIYE BINGWA WA WILAYA YA TEMEKE,USHAHIDI WA PICHA UKO HAPA

Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA JANU. 20,2014 SAA 09:02 USIKU

Ligi ya mpira wa kikapu kwa wilaya ya Temeke(Ligi ya maendeleo ya Temeke) imemalizika siku ya jana(19Jan.2013) kwa mchezo wa
fainali ambapo ilizikutanisha timu ya ABC na timu ya JKT,mchezo uliopigwa katika uwanja wa ndani wa taifa(INDOOR). 
Na katika fainali hiyo timu ya ABC imeibuka na ushindi wa alama 84 kwa alama 60 za JKT.
Kazi ilianza
Kocha wa ABC akitoa maelekezo kwa vijana wake
Viongozi washirikisho la mpira wa kikapu wakibadilishana mawazo
Kabla ya kuanza kota ya tatu mgeni rasmi ambaye ni Rais mpya wa shirikisho la mpira wa kikapu Ing.John Zaniye Bandiye ,alisalimina na wachezaji
Rais mpya wa shirikisho la mpira wa kikapu Ing.John Zaniye Bandiye akifurahi pamoja na kocha wa ABC
Viongozi wakifurahi jambo

Rais mpya wa shirikisho la mpira wa kikapu Ing.John Zaniye Bandiye akitoa nasaa zake kabla ya kuanza kota ya tatu
Timu zikisalimiana kwa ajili ya kuanza kota ya tatu
Mchezo ukaanza tena

Vikombe kwa ajili ya washindi
Mwisho wa mchezo matokeo yakawa hivi
Mmoja wa waamuzi wa mchezo akipokea shukrani zake
Mwamuzi mkuu ,Haleluya Kavarambi pia alikuwepo
Mchezaji mwenye nidhamu
MVP ni Erick Livingston
Mshindi wa pili ni JKT
Mshindi wa kwanza ni ABC
Hongereni sana


Ligi hiyo ilihusisha timu mbalimbali kutoka wilaya ya Temeke,imeandaliwa kwa lengo la timu za wilaya hiyo ziweze kujiandaa na ligi ya mkoa wa Dar es salaam inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments