Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA DISEMBA 6,2013 SAA 11:11 JIONI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Rais
wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela kilichotokea jana (Desemba 5
mwaka huu) nchini humo.
Msiba
huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwa Afrika Kusini,
Afrika na Dunia kwa ujumla kutokana na mchango mkubwa wa Mzee Mandela
katika mchezo huo.
Mzee
Mandela anakumbukwa kwa mchango wake katika Fainali za Afrika (AFCON)
zilizofanyika mwaka 1996 nchini Afrika Kusini na hata zile za Kombe la
Dunia zilizofanyika nchini humo mwaka 2010.
TFF
tunatoa pole kwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA),
Danny Jordan, na wananchi wa Afrika Kusini na kuwataka kuwa na subira
na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mungu aiweke roho ya marehemu Mandela mahali pema peponi. Amina.
0 Comments