Na.Baraka Kizuguto.IMEWEKWA DESEMBA 15.2013 SAA 01:50 USIKU
Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji
wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel
Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.
Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.
Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki
wengi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika
klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa
2015/2016.
Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania
linafungwa leo usiku Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa
kihistoria klabu ya Yanga wamekamilisha taratibu zote za usajili ikiwa
ni pamoja na kupata hati ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.
Usajili
wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji
watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna
Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.
Uongozi
wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano
wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la
usajili.
Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi
karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma Kaseja
ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka
timu ya Ruvu Shooting.
0 Comments