Ticker

6/recent/ticker-posts

BOSS WA MANCHESTER UNITED DAVID MOYES,ANASEMA ALIMUONYA MWENYEKITI WA EVERTON BILL KENWRIGHT

  Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 3.2013 SAA 06:44 USIKU
David Moyes na Bill Kenwright wakati wa siku zao katika klabu ya  Everton
David Moyes amesema kuwa alimuonya mwenyekiti wa sasa wa klabu ya Everton Bill Kenwright kuwa angeweza kuondoka
Everton na baadhi ya wachezaji wake mara baada ya kuteuliwa kuwa meneja wa Manchester United.

Moyes ameitumikia Evaerton kwa miaka 11 kabla ya kuondoka na kuchukua nafasi ya Sir Alex Ferguson katika uwanja wa Old Trafford mwishoni mwa majira ya joto. 

Moyes amewakasirisha mashabiki wa Evarton na  Kenwright baada ya kumchukua na Marouane Fellaini na kumtaka Leighton Baines  kwa ofa,  pamoja £ 28million,kitendo kilichoonekana kuwa ni  "matusi".

Ingawa Fellaini alifanikiwa kuondoka katika tarehe ya mwisho ya siku ya usajili kwa kiasi cha £ 27.5m, Baines yeye alibakia,baada ya  Everton kumkatalia Moyes juu ya jitihada zake hizo katika masaa ya mwisho kabla ya dirisha la uhamisho kufunga.

"Mara baada ya mimi kuanza kazi United, nilijadiliana kwa pamoja na kwa karibu tena mara moja na Bill," alisema David Moyes. 

"Mimi nilimwambia kuwa kuna baadhi ya wachezaji ambao napenda kuwa nao"
"Bill alikuwa anajua lakini ni wazi kuwa mara zote ni kitu kigumu kusema ukweli."  

Hata hivyo David William Moyes inaonekana bado ana maslahi na Baines,kwani gazeti la Sunday Express lililo chapishwa tarehe 27 Oktoba 2013,liliandika kuwa Moyes tayari ameendelea na mpango wake wa kumchukua Baines na amefikia kiasi cha £ 15million katika harakati za kumchukua nyota huyo wa Everton na England  katika dirisha la uhamisho mwezi Januari.


 

Post a Comment

0 Comments