Na.Boniface Wambura,IMEWEKWA NOV. 26,2013 SAA 03:08 USIKU
Mechi
ya kwanza ya raundi ya michuano ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kwa wanawake
chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini iliyokuwa ichezwe
Mwanza sasa itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada
ya ukaguzi uliofanywa na maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), imebainika uwanja huo unatakiwa ufanyiwe marekebisho ambayo hayawezi
kuwahi Desemba 7 mwaka huu, siku ambayo ndiyo mechi hiyo inatakiwa kuchezwa.
Vyumba
vya wachezaji vya uwanja huo ndilo eneo ambalo linatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa.
KILIMANJARO
STARS YATUA SALAMA NAIROBI
Timu
ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imewasili salama Nairobi, Kenya tayari kwa
mashindano ya Kombe la Chalenji yanayoanza kesho (Novemba 27 mwaka huu) katika
Uwanja wa Nyayo.
Kilimanjaro
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iliwasili saa 3 usiku kwa
ndege ya RwandAir, na imefikia katika hoteli ya Sandton iliyoko katikati ya
Jiji la Nairobi.
Kwa
mujibu wa programu ya Kocha Mkuu Kim Poulsen, Kilimanjaro Stars leo (Novemba 26
mwaka huu) ni mapumziko ambapo kesho itafanya mazoezi kujiandaa kwa mechi yake
ya kwanza dhidi ya Zambia itakayochezwa Novemba 28 mwaka huu Uwanja wa
Machakos.
MICHUANO YA
UHAI YAHAMIA CHAMAZI
Michuano
ya Kombe la Uhai imeingia hatua ya robo fainali ambapo sasa mechi zinachezwa
kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam.
Uamuzi
wa kuhamisha mechi hizo kutoka viwanja vya Karume na DUCE ni kuziwezesha zote
kuoneshwa moja kwa moja (live) na Azam Tv.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunaomba radhi kwa washabiki ambao watakuwa
wameathirika kutokana na uamuzi huo.
0 Comments