Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 24.2013 SAA 8:35 MCHANA
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Mh.Ismail Aden Rage (MB) amekataa agizo liliotolewa na Tff la kumtaka kuitisha mkutano
mkuu wa Dharura wa wanachama wake ndani ya siku 14 kuanzia jana.
mkuu wa Dharura wa wanachama wake ndani ya siku 14 kuanzia jana.
Alisababisha foleni katika mtaa wa msimbazi,baada ya mashabiki wa klabu hiyo kutaka japo kumshika mkono |
Akizungumzana waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo,mwenyekiti huyo aliyesimamishwa na kamati ya utendaji ya klabu hiyo,amesema alitegemea kuona kama Tff ingesema kuwa inalaani kitendo cha kufanya mapinduzi kilichofanya na kamati ya utendaji ya Simba Sports Club,badala yake imeitisha mkutano ndani ya siku 14.
"Siitishi mkutano kwa tarehe 14(alikosea kutokana na jazba,ila alikuwa anamaanisha baada ya siku 14) Kama Tff itan'gan'ganiza nitajiuzulu"alisema Mh.Ismail Aden Rage.
Alinukuu vifungu kadhaa vya katiba ya Simba na Tff |
Aidha Mh.Ismail Aden Rage ameongeza kuwa,ibara ya 22 ya klabu ya simba inasema kuwa,mwenyekiti ndio mwenye mamlaka yakuitisha mkutano,lakini kama ataona inafaa au la.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuna mgogoro katika klabu baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.
Pia Rage ameitoa ufafanuzi kuhusiana na swala la Okwi,na amesema swala hilo bado liko mikononi mwa FIFA.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuna mgogoro katika klabu baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Mh.Ismail Aden Rage (MB)akiwasalimu baadhi ya wanachama wa klabu hiyo nje ya makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa msimbazi. |
Na katika swala la Tv. mwenyekiti huyo amesema mwenye haki za Tv ni TFF,ila Simba wa wanapokea tu matokeo kama unataka kuonyeshwa au hutaki.
Pamoja na hayo Rage amemteua Michael Wambura katika kamati ya utendaji ya Simba,nafasi aliyokuwa Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki,sababu ya kufanya hivyo ni Malkia wa nyuki kusema kuwa asingeweza kutumikia nafasi hiyo.
Kwa maaana hiyo Rage amemuomba Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, .

0 Comments