Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 26.2013 SAA 10:21 ALFAJIRI
Mwenyekiti wa mabingwa wa Uropa na Ujerumani, Bayern Munich,
Karl-Heinz Rummenigge, amesema hawatajaribu kumsaini
nyota mkuu Lionel
Messi ambaye analipwa kiasi cha Euro milioni 250 katika klabu yake ya Barcelona. Mwenyekiti wa Klabu ya Beyern Munich Karl-Heinz Rummenigge |
“Tunazungumzia kiasi cha fedha ambacho hatuwezi kumudu, kiasi kikubwa
kuliko zile tulizotoa kumleta Javi Martinez. Hatutasubutu kwenda hapo,”
Rummenigge aliambia runinga ya Ujerumani ya Sky Sports.
“Rais wa Barcelona, Sandro Rosell ni rafiki wa jadi na ninajua hawawezi kumuuza Mess,kwa kuwa ni mtu anayeheshimiwa katika klabu ya Barcelona".
“Ninafikiria itamfaa Messi kubakia Barcelona. Anatosha katika klabu hiyo.”
Fununu za jaribio la kumsaini Messi, biashara ambayo inaweza
muunganisha na mwalimu wake wa zamani, Pep Guardiola, zimekuwa
zikitembea Ujerumani.
Klabu hicho cha Bavaria kina uwezo wa kumudu fedha hizo kuu,kwani
walitangaza wiki mbili zilizopita kuwa wametengeneza Euro million 432.8
kotoka mauzo msimu jana.
“Kwa nini nimsajili Messi? Hapana, hapana, Barcelona ndio mahali panapomfaa zaidi,” ilisema Guardiola.
Bayern waliwacharaza watani wao Borussia Dortmund 3-0 na kusonga alama nne
mbele katika kilele cha Bundesliga huku wakiwa wamefuzu kwenye awamu ya
muondoano ya Ligi ya Mabingwa ya Uropa.
0 Comments