Na.Mohamed Mharizo, IMEWEKWA NOVEMBA 26.2013 SAA 09:21 MCHANA
Baadhi ya washiriki wa kozi ya Ukocha Ngazi ya Pili(Intermediate) wakimsikiliza mkufunzi wa kozi hiyo, Rogasian Kaijage (hayupo pichani) Juni mwaka huu.Kozi hiyo iliendeshwa na DRFA. |
CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
kimezitaka timu zinazoshiriki Ligi Daraja laPili Mkoa wa Dar es Salaam
kuhakikisha makocha wao wanakuwa na taaluma ya ngazi
ya pili (Intermediate) na mikataba ya kazi hiyo.
ya pili (Intermediate) na mikataba ya kazi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa DRFA Kenny Mwaisabula
amesema Dar es Salaam kuwa timu zote zinatakiwa kutekeleza agizo ili kuendana
na malengo ya chama hicho katika kukuza na kuendeleza mchezo huo.
“Tunazitaka timu zote zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili Mkoa
wa Dar es Salaam kuwa na makocha wenye taaluma hiyo Ngazi ya Pili
(Intermediate), tunafanya hivi ili kuendana na dhamira yetu ya kukuza na
kuendeleza mpira wa miguu.
“Kama mtakumbuka vizuri DRFA iliendesha mafunzo ya ukocha wa
Ngazi ya Pili (Intermediate) Juni mwaka huu ikiwa na nia njema ya kuhakikisha
mafanikio yanapatikana, tumekuwa mstari wa mbele na mfano wa kuigwa katika
kuendeleza mpira wa miguu hasa taaluma ya makocha,” alisema.
Alisema timu hizo zimepewa mechi tatu kutekeleza agizo hilo
na iwapo hawatatekeleza zitachukuliwa hatua.
Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam ilianza Novemba 23 ikishirikisha timu 32.
Kamati ya Mashindano ya DRFA inaongozwa na Mwaisabula, wakati
Makamu Mwenyekiti ni Shaaban Mohamed huku wajumbe wakiwa ni Hugo Seseme, Daudi
Kanuti, Kassim Mustapha, Abeid Mziba na Bakari Mtumwa.
0 Comments