Ticker

6/recent/ticker-posts

ALICHOKISEMA KOCHA WA UGANDA,MICHO KUHUSIANA NA EMMANUEL OKWI NA GODFREY WALUSIMBI

Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA NOVEMBA 7.2013 SAA 11:51 JIONI
Emmanuel Okwi na Godfrey Walusimbi
Kocha mkuu wa timu ya Uganda Milutin Sredojević(Micho) amewatetea Emmanuel Okwi na Godfrey Walusimbi kwa
kuwajumuisha katika timu ya maandalizi kwa ajili ya michuano ya CECAFA, ambayo itaanza baadaye mwezi huu mjini Nairobi.

Nyota hao wawili wenye uzoefu, ambao Micho anakusudia kuwanao pamoja katika mashindano ya Chan nchini Afrika Kusini mwezi Januari, ni baadhi ya wachezaji ambao wamerudi nyumbani baada ya kushindikana kucheza soka la kulipwa nchini Tunisia na DRC.
"Nataka kuchukua timu kwa ajili ya Chan yenye mchanganyiko wa uzoefu na vijana," alisema kocha huyo wa Serbia, na kuongeza, "Mimi daima hutoa nafasi ya wachezaji wapya kuja,lakini nahitaji  wale wenye uzoefu kuwasaidia wale wanaokuja"
"Na kama wanacheza vizuri hakuna haja ya kunizui kuongeza katika timu yangu kuwa na wachezaji wa kigeni kuwashilikisha sana katika mashindano ya CECAFA. "

Hata hivyo, bado inaokana kama Okwi na Walusimbi ( bado hawajapata ITC zao), ambapo wamerudi kucheza ligi za ndani mwezi uliopita, wataruhusiwa katika mashindano yajayo ya Chan, mashindano ambayo ni kwa ajili ya wachezaji wa ndani ya nchi.
Okwi ambaye ameuzwa na klabu ya simba kwenda klabu ya Tunisia ya Etoile Du Sahel,lakini mtandao wa supersport.com umeandika kwamba anacheza kwa mkopo katika klabu hiyo, maana yake bado ni mchezaji wa kigeni.
Na mkurugenzi mtendaji wa Fufa Edgar Watson alifafanua kwamba "tunajua kuwa ana haki ya kucheza kwa sababu mamlaka ya FIFA inasema mkopo wake unahoja ya kucheza ndani ya nchi lakini sasa nilazima sisi kwenda kuandika kwao (FIFA) na kuthibitisha," Mkurugenzi Mtendaji Fufa alielezea

Post a Comment

0 Comments