Na.Richard Jules,IMEWEKWA NOV. 14,2013 SAA 10:30 JIONI
TAARIFA YA KUSOGEZWA MBELE LIGI YA MPIRA WA KIKAPU MKOA WA DSM (RBA) 2013/14.
Ndugu Wadau wa Mpira wa KIKAPU Mkoa DSM.
Napenda kuchukua nafasi hii kwa mara nyingine kuwataarifu juu ya
kusogezwa mbele kwa Mashindano ya Ligi ya Mpira wa KIKAPU Mkoa wa Dar Es
Salaam (RBA) kwa msimu wa mwaka 2013/14 yaliyokuwa yakitarajiwa kuanza
siku ya Jumamosi tarehe 16/11/2013.
Chama Cha Mpira wa Kikapu
mkoa wa Dar Es Salaam (BD), baada ya kikao chake cha Bodi kilichokaa na
kutathmini mawazo mbalimbali toka kwa Viongozi na wadau mbalimbali
waliohudhuria Mkutano Maalumu ulioandaliwa na Chama na wadau wa mpira wa
Kikapu DSM yenye nia ya kuongeza Tija katika mchezo wetu ngazi ya Mkoa,
kimefikia Azimio la kusogeza mbele kwa mashindano ya RBA kwa msimu huu
2013/14 mpaka hapo itakapotangazwa tena.
Barua za Taarifa hizi zimekwisha fika Vilabuni na mchakato wa kuzisambaza unaendelea.
Sambamba na hilo.
Viongozi wote wa Vilabu shiriki Ligi ya Mkoa (RBA) 2013/14 mnaombwa
kufika bila kukosa katika Mkutano wa Viongozi wote siku ya Jumanne
tarehe 19/11/2013 kuanzia saa 10:00 jioni katika Ukumbi wa Taasisi ya
Malezi ya Vijana ya DON BOSCO – Upanga.
BD inaomba radhi kwa
usumbufu utakaojitokeza tokana na mabadiliklo hayo, ambayo kimsingi
yamezingatia matakwa ya wadau wa Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar Es Salaam
ili kuweza kuleta Tija katika kuendeleza jitihada za kuboresha Mchezo wa
Mpira wa Kikapu Mkoani na Taifa kwa ujumla.
BD inatambua na
kuthamini michango wa wadau na Ushirikiano utakaoleta ufanisi katika
maendeleo ya mchezo wa Mpira Kikapu Mkoa wa Dar Es Salaam.
IMETOLEWA NA:
Richard Jules. MAKAMU WA RAISI-BD. CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU DSM (BD)
0 Comments