Manchester United imefanya mazoezi bila Michael Carrick, Jonny Evans na Rafael hii leo ambapo wanajianda na mechi ya ligi ya
mabigwa dhidi ya Real Sociedad hapo kesho.
mabigwa dhidi ya Real Sociedad hapo kesho.
Kukosekana
kwa wachezaji hao kuna leta mashaka makubwa juu ya ushiriki wao katika mechi ya kesho, na
shaka kubwa juu ya Carrick baada ya yeye kukosa mechi ya mwishoni mwa wiki ya
Ligi Kuu ambayo walishinda dhidi ya Fulham.
Evans na Rafael aliyeumia kifundo cha mguu walitolewa nje baada ya kuumia katika uwanja wa Craven Cottage na inawezekana kukosa kuruka na ndege kuelekea Hispania na timu.
Mshambuliaji
Danny Welbeck, ambaye alikosa mchezo wa Fulham baada ya kuumia goti, hakuwa katika sehemu ya kikosi kilichofanya mazoezi hii leo kabla ya ndege na chakula cha mchana na kuelekea Hispania.
Mchezeshaji Adnan Januzaj alimeonekana kuwa na maaumivu,ingawa hakuna majibu mabaya ambayo yametolewa kufuatia mgongano wake na Sascha Riether.


0 Comments