IMEWEKWA OKTOBA 30,2013 SAA 8:30 USIKU
Zidane anaonekana kuchukua zaidi utawala katika klabu ya Real Madrid,baada ya
klabu kuthibitisha kumsaini mwanachama wa tano
wa familia ya Zidane.
Ni mtoto mdogo wa Zinedine Zidane anaitwa Eliaz amejiunga na baba yake pamoja na kukutana na ndugu zake watatu Luca, Theo na Enzo katika acadedemy ya Valdebebas,ana umri wa miaka nane ataanza kucheza katika timu ya klabu ya umri chini ya miaka 9 msimu huu.
Kulingana
na tovuti rasmi ya klabu , Eliaz ambaye alizaliwa Marseille
tarehe 26 Desemba 2005,ana uzani 27kg na anasimama katika urefu 1.35m.
Cha kushangaza
kiungo huyo kijana anasema anavutiwa sana na beki Raphaël Varane, na anasema
kuwa mchezo wake ambao hatausahau ni wa mwaka 2010 Mestalla,katika fainali ya kombe la Kihispania , ambapo Real Madrid iliwapiga Barcelona.
Ana nguvu na kipawa cha utaalamu,anatumia mguu wa kushoto,na ana maono makubwa" Tovuti ya klabu ilisema.
Ndugu mkubwa wa wanne, Enzo, anacheza katika timu chini ya miaka 18 na imekuwa katika chuo tangu mwaka 2004. Luca, ambaye anavutiwa na Iker Casillas, ni mmoja wa makipa wa timu ya chini ya miaka 16,kiungo msambuliaji Theo (11), ambao anavutiwa na mchezaji ni Cristiano Ronaldo,yuko katika msimu wake wa nne katika chuo.
Hii ina maana kuna uwezekano wa line-up ya siku zijazo ya Real Madrid akahusisha Zidane wanne pamoja na baba yao Zinedine ambaye anafundisha katika
Uwanja wa Santiago Bernabeu.

0 Comments